Uganda yaripoti visa vipya viwili vya ugonjwa wa Ebola
25 Mei 2026
Uganda imeripoti watu wawili wapya kuwa wameambukizwa Ebola, na kufanya jumla ya maambukizi kufikia saba, huku mamlaka za afya zikisema visa vyote vinahusishwa na mlipuko unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wizara ya Afya ya Uganda imesema wahudumu wawili wa afya katika hospitali binafsi jijini Kampala wamekutwa na maambukizi baada ya kuhusika katika matibabu ya mgonjwa kutoka Kongo aliyefariki mwezi uliopita. Wakati huo huo, nchini Kongo, watu wanaoshukiwa kuambukizwa Ebola wamepindukia 900, hasa katika jimbo la Ituri mashariki mwa nchi. Mlipuko huo umetangazwa kuwa dharura ya afya ya umma ya kimataifa, huku virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo vinavyosababisha ugonjwa huo vikiwa havina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa kwa sasa.