1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yadaiwa kumkatalia Besigye kurudi nyumbani

11 Mei 2011

Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda, Forum for Democratic Change (FDC) kimesema serikali imemzuilia kiongozi wao, Kizza Besigye, asirudi nchini humo kutoka nchi jirani ya Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu.

https://p.dw.com/p/11DUU
Polisi ya UgandaPicha: Simone Schlindwein

Kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho, Anne Mugisha, "vyombo vya usalama vya Uganda vililiambia Shirika la Ndege la Kenya, kwamba kama Besigye atapanda ndege ya shirika hilo, basi hawatairuhusu ndege hiyo kutua nchini Uganda."

Kizza Besigye
Kizza BesigyePicha: AP

Besigye alitarajiwa kurudi leo akitokea matibabuni mjini Nairobi, baada ya kujeruhiwa kwa kipigo cha polisi wa Uganda wakati wa kampeni ya kutembea kwa miguu kwenda kazini, inayokusudia kupinga upandaji wa gharama za mafuta na vyakula jijini Kampala. Watu watano wameuawa kutokana na vurugu baina ya polisi na wapinzani.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Othman Miraji