1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Kizza Besigye

Kizza Besigye ni mwanasiasa kutoka nchini Uganda. Ni kiongozi katika chama kikuu cha upinzani cha Forum for Democratic Change FDC, alichosaidia kukianzisha mnamo mwaka 2001.

Besigye alikuwa moja wa waliopigana katika vita vya msituni vilivyomleta rais wa Uganda Yoweri Museveni mwaka 1986 na alihudumu katika nafasi kadhaa za uongozi kabla ya kufarakana na chama hichi akikituhumu kwa kukiuka misingi na kanuni walizojiwekea wakati wanapamba na tawala zilizopita. Besigye amekuwa kipambana na Museveni katika chaguzi za rais tangu mwaka 2001, na kushindwa na mkongwe huyo, lakini mwenyewe hakubaliani na matokeo ya chaguzi hizo anazodai zinakumbwa na udanganyifu mwingi.

Onesha makala zaidi