1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Uganda: Ruksa wasichana kutumia uzazi wa mpango

11 Oktoba 2023

Mpango wa serikali nchini Uganda kuruhusu wasichana kuanzia miaka 15 kutumia dawa za uzazi wa mpango wapingwa na jamii wakisema hatua hiyo ni kuhalalisha ngono kwa wasichana katika umri mdogo.

https://p.dw.com/p/4XOoZ
Msichana mdogo akiwa mjamzito
Msichana mdogo akiwa mjamzitoPicha: Monicah Mwangi/Reuters

Wazazi, walimu na jamii kwa jumla katika taifa hilo la Afrika Mashariki wamekemea vikali mpango huo wakisema hatua hiyo ni sawa na kuhalalisha ngono kwa watoto wa chini ya umri.

Wamesema mpango huo haujali kwamba wasichana wadogo wanaweza kuambukizwa magonjwa hatari ya zinaa mbali za kuzuwia mimba. 

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya, matumizi ya dawa za uzazi wa mpango maarufu kama Contraceptives ni hatua madhubuti ya kuwalinda wasichana wa rika la kati ya miaka 15 hadi 20 kutozaa watoto ambao hawako tayari kuwatunza.

Soma pia:Wake wa viongozi Afrika himizeni ajenda ya uzazi wa mpango

Aidha ni njia moja ya kuepusha utaoji mimba usio salama ambao umewasababisha wasichana wengi kupoteza maisha yao wanapojaribu kufanya hivyo. 

Mwezi mei mwaka huu, Uganda ilisaini mkataba na shirika la umoja mataifa linaloshughulikia idadi ya watu UNPF kushiriki katika mipango ya kudhibiti uzazi.

Miongoni mwa watoto na vijana na yamkini hili ndilo chimbuko la mpango wa serikali kuanza kuwaruhusu wasicha kuanzia miaka 15 kupata dawa hizo na huduma nyingine za uzazi wa mpango.

Lengo la serikali ni kuzuia mimba au kuzaa watoto ambao msichana au mwanamke hakupanga.

Hata hivyo mpango huo umekabiliwa na vizingiti kutoka kwa wazazi, walimu, viongozi wa kidini  na wanajamii kwa jumla.

Hali ya kuzaliana Uganda 

Kulingana na takwimu za wizara afya na ofisi ya taifa ya takwimu UBOS, zaidi ya nusu ya wanawake na wasichana chini ya umri wa miaka 24 nchini Uganda ni wajawazito au wamekwisha zaa.

Hii ina maana kuwa wengi wao wameshiriki ngono wakiwa na umri mdogo.

Katika kipindi cha zuio ya UVIKO 19 idadi kubwa ya wasichana kati ya umri wa miaka 15 hadi 19 walishika mimba.

Wanafunzi Uganda wakiwa Darasani
Wanafunzi Uganda wakiwa DarasaniPicha: Hajarah Nalwadda/AP Photo/picture alliance

Tangu wakati huo, idadi kubwa ya wasichana imeripotiwa kuacha shule na kuanza majukumu ya kuwalea watoto bila kuandaliwa vyema kama wazazi. 

Naye Bashira Nantongo ambaye ni mhadhiri na mshauri nasaha wa wasichana na wanawake alihoji wakati wanapodhibiti mimba kwa wasichana, vipi wale waliopitia madhira ya kubakwa na kunajisiawa?

Wasichana hawa wanabakwa na watu wazima." Alisema.

Soma pia:Utumiaji holela wa vidonge vya uzazi vya P2 kwa wasichana na hatari inayowakabili

Kulingana na kamishna wa vijana katika wizara ya jinsia na maendeleo ya kijamii Kyateka Mondo, katika kipindi cha UVIKO 19 hadi wasichana 1,000 walikuwa wakishika mimba kila wiki.

Amelezea hali hii kuathiri pakubwa raslimali watu ya Uganda na kuwasababisha mzigo mkubwa kwa wazazi wanaokidhi mahitaji ya  watoto na wajukuu kwa pamoja.

Ni kwa msingi huu ndiyo yeye anaounga mpango wowote unaoweza kudhibiti viwango vya uzazi kwa kutumia dawa za uzazi wa mpango kwa wasichana kuanzia miaka 15.

Vijana hupendelea njia zipi za uzazi wa mpango?

Lakini wadau wanahoji kwa nini serikali haizingatii kwamba si tu mimba za utotoni  ndizo zinahitaji kudhibitiwa lakini pia magonjwa ya kingono.

Kwa upande wao, viongozi wa kidini wanahimiza kuwa ndoa izingatiwe kuwa njia ya pekee ya kumwezesha mtoto wa kikekuwa na mtoto.

Kwa hiyo, njia zozote zile za uzazi wa mpango si sawa. Lubega Emmanuel DW Kampala.