1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mkuu India waingia awamu ya mwisho Jumapili

Oumilkheir Hamidou Emmanuel Derville
17 Mei 2019

Idadi ya wanaoteremka vituoni inasemekana inaridhisha hata hivyo kuna jimbo ambako wapiga kura wanasusia uchaguzi huo-jimbo la Kashmir. Idadi ya walioteremka vituoni katika jimbo hilo inafikia asili mia 22 tu.

https://p.dw.com/p/3Iei5
Indien Westbengalen Wahl
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Das

Uchaguzi mkuu wa India ulioanza tangu April 11 iliyopita unaingia katika awamu yake ya mwisho Jumapili inayokuja. Idadi ya wanaoteremka vituoni inasemekana inaridhisha hata hivyo kuna jimbo ambako wapiga kura wanasusia uchaguzi huo-jimbo la Kashmir, kaskazini mwa nchi hiyo ambako wanaharakati wanaendesha mapambano ya kujitenga tangu miaka 70 sasa. Idadi ya walioteremka vituoni katika jimbo hilo inafikia asili mia 22 tu.

 Ashraf Wani ana umri wa miaka 29. Lakini tangu miaka mitatu iliyopita hawezi tena kufanya kazi wala kuendelea na masomo. Ni shida kwake kuisahau siku moja ya Oktoba mwaka 2016 ambapo alishiriki katika maandamano mjini Pulwama. Vikosi vya usalama vilivyoshamiri bunduki za rashasha vilifyetua risasi za kweli na kumpiga Ashraf machoni.

Sawa na asilimia 78 ya wapigakura, Ashraf anasusia uchaguzi huo. Anaamini wakaazi wa Kashmir wanaangaliwa kuwa ni wakaazi wa tabaka ya pili nchini India.

Wakaazi wa kashimir wanakerwa na zoezi hilo la uchaguzi wanaolilinganisha sawa na dhambi.
Wakaazi wa kashimir wanakerwa na zoezi hilo la uchaguzi wanaolilinganisha sawa na dhambi.Picha: picture alliance/Pacific Press/F. Khan

"Kawaida, kama kuna maandamano, polisi wanatumia mbinu hiozo hizo. Naiwe Mumbai, naiwe Delhi au katika majimbo yote  mengine ya India, polisi wanatumia zana nyengine mfano mabomba ya maji au maguruneti yanayowafanya watu wasiweze kusikia. Lakini katika jimbo la Kashmir, vikosi vya usalama vinefyetua bunduki za rashasha zenye risasin za kweli dhidi ya raia. Kwa namna hiyo tunaona vizuri kabisa kwamba  jimbo la Kashimir haalitendewi sawa nma majaimbo mengine."

Upinzani dhidi ya mfumo wa kisiasa umeanza mwaka 2016 pale jeshi lilipomuuwa Burhani Wani, mwanaharakati aliyekuwa mashuhuri sana mitandaoni. Miezi iliyofuatia wanajeshi wakawafyetulia risasi waandamanaji -watu wasiopungua 14 waliuwawa na wengine 3000 kujeruhiwa.

Idadi ya walioteremka vituoni katika jimbo hilo inafikia asilimia 22 tu.
Idadi ya walioteremka vituoni katika jimbo hilo inafikia asilimia 22 tu.Picha: Reuters

Mfarakano ulizidi makali baada ya shambulio dhidi ya magari ya wanajeshi huko Pulwama, shambulio lililoangamiza maisha ya watu 40 mwezi wa Feburuari na ambalo kundi la wafuasi wa itikadi kali kutoka Pakistan lilidai kuhusika. Wakaazi wa Kashimir ndio waliolipiziwa kisasi cha shambulio hilo.

Hata vyama vya kisiasa vya Kashimir havithaminiwi kama anavyosema Naeem Akhter wa chama cha PDP.

"Tulipofanya kampeni kwaajili ya uchaguzi wa bunge hatukuweza kubanadika mabango wala kutundika bendera za chama.Tungefanya hivyo wafuasi wetu wangekaabiliana na ghadhabu za wanaharakati."

Wakaazi wa kashimir wanakerwa na zoezi hilo la uchaguzi wanaolilinganisha sawa na dhambi.