1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ubalozi wa Marekani wafungwa Kinshasa kwa hofu za shambulizi

Sekione Kitojo
29 Novemba 2018

Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa umeendelea kufungwa kwa siku ya nne leo , baada ya Marekani kuonya kuhusiana na uwezekano  wa  kitisho cha ugaidi dhidi ya ubalozi huo.

https://p.dw.com/p/397Ia
Demokratische Republik Kongo Stadt Kinshasa Panorama
Picha: AP

Ubalozi  wa  Marekani  mjini  Kinshasa  umeendelea kufungwa  kwa  siku  ya  nne  leo , baada  ya  Marekani kuonya  kuhusiana  na  uwezekano  wa  kitisho  cha  ugaidi dhidi ya  ubalozi  huo  katika  jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya Congo.

Raia  wa  Marekani  mjini  Kinshasa  pamoja  na  maeneo mengine  ya  Congo  wanatakiwa  kuchukua  tahadhari  na kuwa  macho  katika  hali  mbali  mbali, ubalozi  huo umesema.

Ubalozi  huo  ulifungwa  siku  ya  Jumatatu. wakati makundi  kadhaa  ya  wanamgambo  yanapigana  nchini Congo, kwa  misingi  ya  kikabila  ama  kuhusiana  na utajiri  wa  madini  nchini  humo, ambapo  mara  kadhaa wafanyakazi  wa  nje  wa  mashirika  ya  misaada wakikumbana  na  matatizo  katika  mzozo  huo, si  kawaida kwamba  Marekani  inaweza  kukabiliwa  na  kitisho  hicho.