1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akutana na wataalam wa teknolojia ya mawasiliano

15 Desemba 2016

Rais mteule wa Marekani Donald Trump na wataalam wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano wako katika nafasi ya kulainisha msuguano na tofauti walizokuwa nazo katika kipindi cha kampeni za urais nchini humo.

https://p.dw.com/p/2UIuR
USA Treffen Donald Trump mit Vertretern der Technologie-Industrie
Picha: Getty Images/AFP/T.A. Clary

Rais mteule Trump alikutana na viongozi hao kwa mazungumzo, vyanzo vinasema kuwa kikao hicho kinaweza kuwasahaulisha juu ya mambo mbalimbali kuhusu Trump ambae ameyalaumu makampuni ya teknolojia ya mawasiliano kwa kuwa katika nafasi ya juu kabisa.

Kikao hicho kinafanyika wakati ambapo kiongozi huyo kutoka chama cha Republican akiwa katika kusubiri, anaendelea kulijaza baraza lake la mawaziri, amemteua gavana wa zamani wa jimbo la Texas Rick Perry kutumikia wadhifa wa waziri wa nishati.

Katika taarifa yake mtendaji mkuu wa kampuni ya Oracle, Safra Catz ambaye pia alihudhuria mazungumzo hayo amesema, kama ataweza kufanyia kazi mabadiliko kanuni ya kodi, kupunguza udhibiti na kujadili mipango bora ya biashara, teknolojia nchini Marekani itakuwa imara na ya ushindani zaidi kuliko ilivyowahi kutokea awali.

Makampuni maarufu ya kiteknolojia kama vile Apple, facebook na Tesla Motors yalipata nafasi ya kutangaza vipaumbele vyao kama vile mfumo wa kubadilisha taarifa kwenda katika kanuni maalum ambayo itadhibiti kupatikana kwa taarifa kwa mtu ambaye hajaruhusiwa na pia ulinzi wa maudhui ya watumiaji wake.

Google Logo Symbolbild
Nembo ya google, moja kati ya kampuni maarufu ya teknolojia na mawasilianoPicha: picture-alliance/dpa/O. Spata

Athari za Urais wa Trump katika sekta ya teknolojia na mawasiliano ni ngumu kutabilika, wakati huo kukiwa na uwezekano wa sekta hiyo kupinga mipaka yoyote ya kibiashara pamoja na ukomo wa wahamiaji. Makampuni mengi yanatarajiwa kuunga mkono masuala kadhaa kama vile kupunguzwa kwa viwango vya kodi kwa makampuni hasa katika faida ambayo inapatikana kutoka nje ya nchi.

Kwa upande mwingine, kuna uwezekano wa kuwepo kwa mvutano kati ya Trump na sekta hiyo katika suala la kuthibiti wa upatikanaji wa taarifa ya ujumbe wa siri unaotumwa kupitia katika mitandao, na uwezo wa maafisa wa usalama na idara za ujasusi kuweza kutumia taarifa hizo kwa kutumia vifaa maalum kubaini ujumbe  na kuendesha uchunguzi katika masuala ya usalama wa kitaifa.

Trump kwa upande wake amesema, uongozi wake utakuwa ukifanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya kibiashara na kufanya kuwa ya kuvutia kwa makampuni ili kutengeneza nafasi mpya za kazi nchini Marekani.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/Reuters/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu