1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump agoma kurudi mahakamani

11 Desemba 2023

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ameamua kutokujitokeza tena mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi ya udanganyifu inayomkabili, akisema ushahidi alioutowa mwezi uliopita umetosha.

https://p.dw.com/p/4a03m
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, amekataa kurejea mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi dhidi yake.
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, amekataa kurejea mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi dhidi yake.Picha: Joe Raedle/AFP/Getty Images

Akiandika kwenye mtandao wake wa kijamii uitwao Truth Social, bilionea huyo anayetaka kuteuliwa na chama chake cha Republican kuwania tena urais mwakani, amesema ameshatowa ushahidi wa kutosha na hana cha kuongeza.

Soma zaidi: Donald Trump anakabiliwa na msururu wa kesi za uhalifu, lakini anakana kufanya kosa lolote

Trump alikuwa anatakiwa kuhudhuria kikao chengine cha mahakama siku ya Jumatatu (Disemba 11) kwenye kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwanasheria Mkuu wa New York, Letitia James.

Mwanasheria huyo anamtuhumu Trump kwa kutia chumvi kwenye taarifa zake za kifedha ili kujipatia mikopo na mikataba ya biashara.

Kesi hiyo inatishia kuiporomosha biashara ya ujenzi ya Trump na kuiharibu taswira yake kama mfanyabiashara aliyefanikiwa.