TOKYO: Chama tawala Japan chapoteza wingi | Habari za Ulimwengu | DW | 29.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO: Chama tawala Japan chapoteza wingi

Vyombo vya habari nchini Japan vinaripoti kuwa Waziri Mkuu Shinzo Abe anatazamia kubakia mdarakani.Hiyo licha ya matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa Baraza Kuu la Bunge,uliofanywa hii leo kuonyesha kuwa chama chake cha LDP kimeshindwa vibaya.

Wagombea kura katika uchaguzi wa leo hii wamepigania nusu ya viti 242 katika Baraza Kuu la Bungeni.Serikali ya mseto itabakia madarakani hata ikipoteza wingi wake katika baraza hilo kwa sababu ina wingi katika Baraza Dogo Bungeni.

Abe,alieshika madaraka miezi kumi iliyopita amepoteza umaarufu wake kwa sababu ya kashfa mbali mbali serikalini,ikiwa ni pamoja na ile inayohusika na malipo ya pensheni ya uzeeni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com