Tanzania: Lema aachiwa kwa dhamana | Matukio ya Afrika | DW | 06.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Tanzania: Lema aachiwa kwa dhamana

Baada ya kukaa rumande kwa miezi minne mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema ameachiwa huru baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumpa dhamana. DW imezungumza na wakili wake Peter Kibatala

Dhamani hiyo ni ya bondi ya shilingi milioni moja za kitanzania na sharti la kuwekewa bondi na wadhamini wawili ya shilingi milioni moja kila mmojaKadhalika ametakiwa pia kuahidi  kufika mahakamani katika kesi ya msingi ya uchochezi inayomkabili. Pamoja na hilo masuali mengi yanaulizwa kuhusiana na suala hili ikiwa ni pamoja na mazingira ya kuachiwa kwake, na kutokana na hilo DW imemtafuta wakili wa mwanasiasa huyo Peter Kibatala na kwanza kuumuuliza Lema ameachiwa katika mazingira gani.

DW inapendekeza