1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu wanne wameuwawa Lebanon kwa mashambulizi ya Israel

25 Aprili 2026

Takriban watu wanne wameuawa nchini Lebanon Jumamosi kutokana na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel kusini mwa nchi hiyo licha ya makubaliano ya kusitisha vita kurefushwa.

https://p.dw.com/p/5CoL6
Mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon 23.04.2026
Moto ukifuka baada ya mashambulizi ya Israel kusini mwa LebanonPicha: Gil Eliyahu/REUTERS

Kulingana na vyanzo vya kiusalama, mashambulizi mawili yalilenga lori na pikipiki kwenye mji wa Yohmor. Tukio hilo linaibua mashaka mapya kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya kuweka chini silaha katika eneo hilo ambalo limekumbwa na mapigano ya mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.

Israel yadai ilijihami na kitisho cha mashambulizi ya Hezbollah

Jeshi la Israel limesema lilishambulia mifumo ya Hezbollah ya kufyetulia maroketi iliyokuwa tayari kwa mashambulizi katika maeneo matatu kusini mwa Lebanon.

Chini ya makubaliano ya sasa ya kusitisha vita,Israel inaruhusiwa kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kupangwa, yanayokaribia kufanywa  au yanayoendelea. Hata hivyo inategemewa kujiepusha na mashambulizi mapya yasiyo na kusudi la kujilinda ndani ya Lebanon.