1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria kuisaidia Marekani kupambana na makundi ya wanamgambo

13 Novemba 2025

Mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Syria Tom Barrack, amesema Syria itakuwa na jukumu muhimu katika kuisaidia nchi yake kupambana na makundi yaliyo na silaha.

https://p.dw.com/p/53YuR
Mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Syria Tom Barrack
Marekani yasema Syria itaisaidia kupambana na makundi ya wanamgambo Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Makundi hayo ni pamoja na Kikosi Maalum cha Walinzi wa Mapinduzi cha Iran, makundi ya wanamgambo ya Hamas na Hezbollah.

Muda mfupi baada ya ziara ya Rais wa Syria, Ahmed al-Sharaa, kwenye Ikulu ya Marekani, White House, muungano unaoongozwa na Marekani kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS ulitangaza kuwa Syria imejiunga na muungano huo na hivyo kuwa mwanachama wake wa 90.

Barrack alindika katika mtandao wake wa X kwamba Syria itasaidia kuyasambaratisha mabaki ya IS na mitandao mengine ya kigaidi.

Kikosi kilicho na nguvu cha Walinzi wa Mapinduzi cha Iran, IRGC na wanamgambo wa Lebanon Hezbollah waliiunga mkono kwa kiasi kikubwa serikali ya rais aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad.