Somaliland yakanusha madai kuwa itawahifadhi Wapalestina
2 Januari 2026
Wiki iliyopita Israel ilikuwa nchi ya kwanza kuitambua Somaliland kama "taifa huru", hatua iliyozusha upinzani kote Somalia. Siku ya Jumatano, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, akinukuu ripoti za kijasusi, aliambia televisheni ya Al Jazeera kwamba Somaliland imekubali masharti matatu kutoka kwa Israel ambayo ni: kuwahamisha Wapalestina, kujengwa kwa kambi ya kijeshi kwenye Ghuba ya Aden, na kujiunga na Makubaliano ya Abraham ili kurekebisha uhusiano na Israel.
Wizara ya mambo ya nje ya Somaliland ilikataa masharti mawili ya kwanza. Ilisema makubaliano yake na Israel yalikuwa ya kidiplomasia tu. Somaliland ilijitangazia uhuru wake mwaka wa 1991 na imekuwa na utulivu na amani zaidi kuliko sehemu iliyobaki za Somalia ambayo imekumbwa na migogoro. Somaliland ilianzisha uchaguzi wake, sarafu na hata jeshi.