1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Somalia yakasirishwa na ziara ya Gideon Saar Somaliland

7 Januari 2026

Serikali ya Somalia imekasirishwa na ziara ya Waziri wa Mambo ya nje wa Israel Gideon Saar, ikiitaja ziara hiyo kama "uvamizi haramu" na "usioidinishwa."

https://p.dw.com/p/56QcK
Brüssel 2025 | Gideon Saar
Waziri wa Mambo ya nje wa Israel Gideon SaarPicha: Nicolas Tucat/AFP

Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia imesema "inahifadhi haki ya kuchukua hatua zote zinazofaa za kidiplomasia na kisheria ili kulinda mamlaka yake, umoja wa kitaifa na uadilifu wa eneo lake."

Somalia imekuwa ikisisitiza kwa miaka mingi kwamba Somaliland ni sehemu isiyotenganishwa ya ardhi yake, na hatua yoyote ya kuitambua inakiuka sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya mataifa.

Mkutano maalum wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika jana Jumanne umelaani vikali uamuzi wa Israel wa kuitambua Somaliland na kuhimiza uamuzi huo "ufutwe mara moja."

Hata hivyo uamuzi wa Israel umeuungwa mkono na Marekani, japo umekosolewa na Misri, Uturuki, Baraza la Ushirikiano la Ghuba lenye nchi sita, pamoja na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu lenye makao makuu yake Saudi Arabia. Umoja wa Ulaya umesisitiza kuwa mamlaka ya Somalia yanapaswa kuheshimiwa.