SiasaAsia
Rais Xi wa China anaanza ziara Korea Kaskazini
8 Juni 2026
Matangazo
Hiyo itakuwa ziara ya kwanza ya Xi nchini Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka saba iliyopita.
Katika makala iliyoandikwa na kiongozi huyo wa China na kuchapishwa leo hii, Xi amesema ni sera isiyoyumba ya utawala mjini Beijing kuimarisha mahusiano na Korea Kaskazini. Pia amesema nchi hizo mbili zitafanya kazi pamoja kupambana na tabia za ubabe na kuongezeka mbio za kuunda silaha mambo aliyoyataja kuwa kitisho kwa usalama na udhabiti wa kanda hiyo.
Akiwa mjini Pyongyang, Xi atakutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ambaye alikutana naye mara ya mwisho Septemba mwaka jana alipomwalika Kim nchini China kwa gwaride kubwa la kijeshi.