1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raila Odinga amteua Martha Karua kama mgombea mwenza

16 Mei 2022

Mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, amemteuwa mwanasiasa mwanamke wa siku nyingi nchini humo, Martha Karua kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi wa Agosti tisa.

https://p.dw.com/p/4BMVF
Kenia Politikerin Martha Karua
Picha: Joan Pereruan/Nation Media Group/dpa/picture alliance

Odinga ameutangaza uteuzi wake muda mfupi uliopia katika kitua cha mikutano cha KICC katikati mwa jiji la Nairobi.

Awali, mpinzani wa Raila Odinga anayeongoza muungano wa Kenya kwanza, William Ruto, alimteuwa Rigathi Gachagua kuwa mgombea mwenza.

Leo ilikuwa siku ya mwisho iliyowekwa na Tume huru ya mipaka na uchaguzi ya Kenya, kwa wagombea urais kuwa wamewateuwa wagombea wenza watakaokuwa manaibu rais ikiwa mgombea wao mkuu utashinda uchaguzi ujao.