1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Qatar yasema Israel na Hamas hawakaribii muafaka kuhusu Gaza

Josephat Charo
12 Machi 2024

Israel na Hamas karibu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachia huru mateka, ikitahadharisha kuwa hali bado ni tete katika uwanja wa vita.

https://p.dw.com/p/4dRHe
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-AnsariPicha: Imad Creidi/REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari amesema hawaoni Israel na Hamas wakizungumza kwa kauli moja.

"Hali ni tete katika uwanja wa vita. Hatujakaribia kupata mkataba kwa maana kwamba hatuoni pande zote mbili zikizungumza lugha moja inayoweza kusuluhisha kutoelewana kulikopo sasa kuhusu utekelezaji wa mkataba wa kusitisha mapigano. Lakini bado tunabaki kuwa n amatumaini na tutaendelea kushinikiza kupatikane mkataba katika siku chache zijazo.", alisema Ansari.

Ansari ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa pande zote zinaendelea kufanya mashauriano kwa matumaini ya kuafikia makubaliano katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Amesema Qatar inafanya kila linaloweza kuzishinikiza pande zinazohasimiana ziafikiane.