1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Putin asema yuko tayari kutumia silaha za Nyuklia

Saumu Mwasimba
13 Machi 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema yuko tayari kutumia silaha za Nyuklia ikiwa kuna kitisho dhidi ya uhai wa nchi hiyo, mamlaka au Uhuru wake.

https://p.dw.com/p/4dSWB
Urusi| Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema yuko tayari kutumia silaha za Nyukliaikiwa kuna kitisho dhidi ya uhai wa nchi hiyo, mamlaka au Uhuru wake.

Katika kauli aliyoitowa kupitia mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha televisheni ya taifa, yaliyorushwa leo Jumatano, Putin amesema anatarajia kwamba Marekani itaepusha kuongeza mgogoro wowote unaoweza kuchochea vita vya silaha za Nyuklia.

Rais huyo wa Urusi amesisitiza  vikosi vyake vya kutumia silaha hizo viko tayari lakini pia alipoulizwa ikiwa amewahi kufikiria kutumia silaha za Nyuklia katika uwanja wa  vita nchini Ukraine, alisema hakuna haja ya kufanya hivyo.

Vile vile amesema ana imani Moscow itafanikiwa kutimiza malengo yake katika vita hivyo vya Ukraine na kwamba mlango wa mazungumzo uko wazi. Amesisitiza kwamba makubaliano yoyote yatahitaji kwanza ahadi thabiti kutoka nchi za Magharibi.