Pompeo ziarani Jerusalem | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.05.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Pompeo ziarani Jerusalem

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliyeko ziarani Mashariki ya kati ametowa matamshi makali dhidi ya Iran akiishutumu nchi hiyo kwa kutumia raslimali zake kuchochea ugaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Pompeo ametowa kauli hiyo leo Jumatano akiwa mjini Jerusalem Israel kabla ya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Pompeo akiishutumu Iran amesema hata katika wakati huu wa janga la mripuko wa kirusi cha Corona Wairan wanatumia raslimali za utawala wa Ayattolah kuchochea ugaidi kote duniani hata pale ambapo watu wa taifa hilo wanapambana.Pompeo ameongeza kusema kwamba hali hiyo inaonesha mengi kuhusu nafsi za wale wanaoiongoza nchi hiyo ya ghuba ya uajemi.

Ziara ya Pompeo nchini Israel ni ya kwanza nchi za nje katika kipindi cha karibu miezi miwili kutokana na janga la Covid-19. Lakini Mwanadiplomasia huyo wa Marekani hakuonekana kuvaa barakoa pale alipokutana na Netanyahu katika ofisi ya waziri mkuu huyo. Na waziri Netanyahu amesema kwamba ziara hiyo ya siku moja ni ushahidi juu ya uimara wa ushirika wao.

Waziri mkuu Netanyahu nae pia hakuisaza Iran,ameisifu sana serikali ya Marekani mjini Washington kwa kuendelea kuitia kishindo Iran,nchi anayodai inaendelea na mipango yake ya matumizi ya nguvu dhidi ya Wamarekani, Waisrael na kila mmoja katika ukanda huo.

Westjordanland | Israelische Siedlung Har Homa

Makazi ya Israel kama yanavyoonekana

Viongozi hao wawili wanatarajiwa pia kujadiliana kuhusu baraka za Marekani katika kuridhia mpango wa Israel wa kutaka kunyakuwa maeneo zaidi katika ardhi iliyoikalia kwa mabavu ukingo wa Magharibi na kutanua makaazi ya walowezi wa kiyahudi.

Ni hivi karibuni tu ambapo hatua hiyo ya kunyakuliwa kwa nguvu kwa maeneo ya wapalestina Ukingo wa Magharibi ilifafanuliwa kwa kina katika mpango wa rais Donald Trump wa amani ya Mashariki ya kati mpango uliogubikwa na utata mkubwa na uliokataliwa kweupe kwa dhati kabisa na Wapalestina.Sera ya ujenzi wa makazi ya walowezi yalaaniwa vikali

Nchi nyingine zenye nguvu duniani zinaiangalia hatua ya Israel ya kunyakua ardhi ya Wapalestina Ukingop wa Magharibi itasababisha kuongeza ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa na kuzima matumaini ya mzozo huo kutatuliwa kwa njia ya kuundwa madola mawili.

Ama katika ziara hii ya Pompeo,waziri mkuu Netanyahu na mshirika wake mpya katika serikali ya mseto ambaye ni kiongozi wa chama cha Buluu na Nyeupe Benny Gantz wameamua kuiaghirisha hafla ya kuapishwa kuingia madarakani hadi kesho alhamisi,ili wapate wasaa wa kukaa na Netanyahu. Kwa maana hiyo Pompeo amepangiwa baade kukutana na Gantz na Gabi Ashkenazi ambaye anatarajiwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Israel.

Ziara ya Netanyahu inafanyika katika wakati ambapo pia zinafanyika vurugu na leo Jumatano ghasia zimezuka Kusini mwa ukingo wa magharibi na kijana mmoja wakipalestina amepigwa risasi ya kichwa na kuuwawa katika makabiliano na wanajeshi wa Israel karibu na mji wa Hebron na vijana wanne wengine wakajeruhiwa. jana mwanajeshi mmoja wa Israel aliuwawa kwa kupigwa jiwe la kichwa. Lakini si Netanyahu wala Pompeo aliyeligusia suala hilo.Na wala jeshi la Israel halijatoa tamko lolote.