1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Haley ajitoa kinyan'ganyiro cha kuwania tiketi ya Republican

6 Machi 2024

Vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa mgombea wa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu Nikki Haley anapanga kusitisha kampeni yake leo.

https://p.dw.com/p/4dEcc
Mgombea wa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu Nikki Haley
Mgombea wa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi wa Novemba mwaka huu Nikki HaleyPicha: Joseph Prezioso/AFP/Getty Images

Uamuzi wa Haley utamuacha Donald Trump kama mgombea pekee wa chama hicho.

Rais huyo wa zamani na mrithi wake, Mdemokrati Joe Biden, wamepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mchujo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, maarufu kama Jumanne Kuu, na ndiyo wanaopewa nafasi kubwa ya kuteuliwa na vyama vyao kuwania urais.

Soma pia: Kinyang´anyiro cha ´Jumanne Kuu´ chawadia Marekani 

Haley, ambaye pia alihudumu kama Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa chini ya Trump, aligeuka mpinzani wake mkuu  katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa chama cha Republican.

Hata hivyo katika kura zilizopigwa jana, Trump alishinda majimbo 14 kati ya 15, yakiwemo Texas na California, huku Haley akishinda katika jimbo moja tu la Vermont.

Haley anatarajiwa kutangaza kumuidhinisha Trump, lakini pia kumuhimiza atafute uungwaji mkono wa wapiga kura wa Republican na wale wa kujitegemea.