1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wengi wameathiriwa vita vya Ukraine, Urusi

28 Januari 2026

Ripoti ya Kituo cha mafunzo ya Kimataifa na ya Kimkakati CSIS, imesema jumla ya wanajeshi waliouawa, kujeruhiwa au waliopotea katika vita ya Urusi dhidi ya Ukraine huenda ikafikia milioni 2 kufikia msimu wa machipuko.

https://p.dw.com/p/57cyk
Ukraine, 25.03.2025
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika kwenye mazoezi karibu na eneo la DonbassPicha: Igor Burdyga/DW

Ripoti ya kituo hicho chenye makao yake Washington, imeeleza kuwa takriban wanajeshi milioni moja na laki mbili wa Urusi wameathiriwa na vita na 325,000 miongoni mwao wameuawa. Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa na taifa lolote kubwa tangu vita vyapili vya dunia.

Vifo vya wanajeshi wa Ukraine ni zaidi ya 140,000

Kwa upande wa Ukraine wanajeshi 500,000 hadi 600,000 wameathiriwa na mapigano huku idadi ya vifo ikitajwa kuwa wanajeshi 140,000 kwa mujibu wa ripoti hiyo. 

Licha ya kupoteza wanajeshi wengi Urusi imefanikiwa kusonga mbele na kujinyakulia maeneo ya Ukraine. Mataifa hayo bado yanakabiliana vikali kwenye uwanja wa mapambano huku juhudi za kuvimaliza vita vilivyodumu kwa karibu miaka minne zikiendelea.