1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanaharakati afungwa kwa kukosoa uvamizi wa Urusi Ukraine

Amina Mjahid
27 Februari 2024

Mwanaharakati mashuhuri wa kupigania haki za binaadamu nchini Urusi Oleg Orlov amehukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela, kwa kukosoa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cxVz
Urusi | Denis Chuprikov
Denis Chuprikov Picha: Sergei Fadeichev/dpa/picture alliance

Mwanaharakati mashuhuri wa kupigania haki za binaadamu nchini Urusi Oleg Orlov amehukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela, kwa kukosoa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Mahakama moja ya mjini Moscow imemkuta na hatia Orlov mwenye umri wa miaka 70, kwa madai ya kulikosoa mara kwa mara jeshi la Urusi.

Soma pia: Mshirika wa Putin akutana Raul Castro wa Cuba kujadili ushirikiano wa usalama

Mkanda wa vidio uliotolewa na shirika la Memorial la Tuzo ya amani ya Nobel ambaye Orlov aliwahi kuwa mwenyekiti wake, ulimuonesha mwanaharakati huyo akifungwa pingu mahakamani baada ya uamuzi huo kutolewa.

Mwaka 2022 Orlov alivipinga kwa uwazi vita vya Urusi nchini Ukraine akiandika nakala iliyopewa jina na " walitaka ufashisti na wakaupata" na kuelezea madhila wanayopitia raia wa Ukraine kuokana na vita hivyo.