1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshirika wa Putin, Castro wajadili ushirikiano wa usalama

Amina Mjahid
27 Februari 2024

Katibu wa Baraza la Usalama la Urusi Nikolai Patrushev, ambaye ni mshirika mkuu wa Rais Vladimir Putin, amekutana na rais wa zamani wa Cuba Raul Castro kujadili kuhusu ushirikiano wa kiusalama.

https://p.dw.com/p/4cvSj
Cuba | Rais wa zamani Raul Castro
Rais wa zamani wa Cuba Raul CastroPicha: Ramon Espinosa/AP/picture alliance

Taarifa ya baraza hilo iliyoonekana na shirika la habari la Urusi, Interfax imeeleza kuwa masuala mengine mengi ya ushirikiano katika nyanja ya usalama yalijadiliwa. Patrushev alimuhakikishia Castro kwamba Urusi inajitolea kubakia kuwa mshirika wa kimkakati baina ya mataifa hayo mawili.

Baada ya nchi hizo za Magharibi kuiwekea vikwazo Urusi, ambavyo Marekani na viongozi wa Ulaya wamevielezea kama vikwazo vilivyo na nguvu kuwahi kuwekewa taifa lolote kubwa, Urusi imejiweka kando na Ulaya na Marekani na kuanza kuimarisha uhusiano wake na nchi za Asia, Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini.

Putin tayari ana mualiko wa kuitembelea Cuba.