1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msukumo wa Israel na Hamas kusitisha mapigano unazidi

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2024

Wapatanishi wa kimataifa na wajumbe wa Hamas wanaendelea na mazungumzo mjini Cairo nchini Misri, ya kujaribu kufikia makubaliano ya usitishaji vita kwa muda katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dAn2
Misri Cairo | Antony Blinken na Abdel-Fattah al-Sisi
Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Cairo, Misri, Februari 6, 2024.Picha: Egyptian Presidency/Xinhua/picture alliance

Wapatanishi wa kimataifa na wajumbe wa Hamas wanaendelea na mazungumzo mjini Cairo nchini Misri, ya kujaribu kufikia makubaliano ya usitishaji vita kwa muda katika Ukanda wa Gaza, kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan mapema wiki ijayo. Wajumbe wa Hamas na wale wa Marekani, wanatarajia kukutana na wapatanishi kutoka Qatar na Misri katika siku ya tatu ya majadiliano ya kufikia makubaliano ya kusitisha vita kwa wiki sita. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kubadilishana mateka waliosalia na mamia ya wafungwa wa Kipalestina sambamba na usambazaji wa misaadaya kiutu Gaza. Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba wajumbe wa nchi hiyo wamesusia mazungumzo hayo baada ya kundi la Hamas kushindwa kutoa orodha ya mateka ambao bado wako hai.