1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mpigania demokrasia Lai atiwa hatiani Hong Kong

16 Desemba 2025

Jimmy Lai, bilionea aliyekuwa akimiliki yombo vya habari na mkosoaji mkubwa wa utawala wa China, ametiwa hatiani kwenye kesi ya aina yake kuhusiana na usalama wa taifa, hukumu ambayo inampeleka jela maisha.

https://p.dw.com/p/55Pgu
Hongkong 2020 | Jimmy Lai Chee-ying
Jimmy Lai, mkosoaji mkubwa wa serikali ya China, ametiwa hatiani kwa kosa la kuhatarisha usalama wa taifa mjini Hong Kong.Picha: Lui Siu Wai/Xinhua/IMAGO

Majaji wa Mahakama ya Hong Kong waliamua jioni ya Jumatatu (Disemba 15) kwamba Lai, mwenye umri wa miaka 78, ana hatia ya kula njama na wenzake kwa kushirikiana na wageni kuhatarisha usalama wa taifa na kuchapisha makala za uchochezi.

Lai, aliyekamatwa kwa mara ya kwanza Agosti 2020 chini ya sheria kali ya usalama iliyoanzishwa na utawala wa Beijing, amekuwa akina makosa hayo.

Kwa muda wa miaka mitano, mpiganiaji huyo wa demokrasia amekuwa kizuizini, sehemu kubwa zaidi akiwa ametengwa, huku familia yake ikisema afya yake imekuwa ikidorora kwa haraka.