1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Moscow yadai kudhibiti kijiji cha mashariki mwa Ukraine

28 Aprili 2024

Wizara ya ulinzi ya Urusi imedai kuwa vikosi vya nchi hiyo vimechukua udhibiti wa kijiji kingine mashariki mwa Ukraine, mnano wakati vikosi vyake vikizidisha mashambulizi kwenye uwanja wa vita.

https://p.dw.com/p/4fGyM
Vita vya Ukraine
Wakaazi wa Donetsk wakipiga foleni kupokea misaada ya chakulaPicha: Narciso Contreras/Anadolu/picture alliance

Moscow

Wizara ya ulinzi ya Urusi imedai kuwa vikosi vya nchi hiyo vimechukua udhibiti wa kijiji kingine mashariki mwa Ukraine, mnano wakati vikosi vyake vikizidisha mashambulizi kwenye uwanja wa vita. Kijiji hicho kinapatikana kilometa karibu 10 kaskazini mwa mji wa Avdiivka, uliodhibitiwa na Moscow mnamo mwezi Februari baada ya mashambulizi makali ya umwagaji damu katika vita vya miaka miwili.

Vikosi vya Urusi vimepata mafanikio makubwa katika eneo la mashariki la mkoa wa Donetsk wiki iliyopita na kusababisha ukosoaji wa nadra kutoka kwa wanablogu wa kijeshi wa Ukraine juu ya vikosi vya nchi hiyo.

Blogu moja katika mtandao wa Telegram ya Deep State, ambayo ipo karibu na wanajeshi wa Ukraine, mapema wiki hii iliwalaumu viongozi wa kijeshi kutokana na kuzorota hali ya usalama katika eneo hilo na kusababisha hasara kubwa.