Matangazo
Kulingana na polisi wa eneo hilo, Daunte Wright mwenye umri wa miaka 20 alisimamishwa na polisi waliokuwa na waranti ya kumkamata dereva wa gari alilokuwa anaendesha, na walipojaribu kufanya hivyo Daunte alirejea kwenye gari na kutaka kutoroka na ndipo polisi walipompiga risasi. Amina Abubakar amezungumza na Dr. Nicholas Boaz mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Marekani kutoa tathmini yake juu ya muaaji hayo.