1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mkuu wa ujasusi wa Israel kujadili usitishaji vita Gaza

18 Machi 2024

Mkuu wa ujasusi wa Israel wajumbe wa Misri na waziri mkuu wa Qatar wanatarajiwa kukutana mjini Doha kwa ajili ya mazungumzo juu ya kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4drwp
Mkuu wa ujasusi wa Israel David Barnea kukutana na wajumbe wa Misri na Qatar katika juhudi za kusitisha mapigano Ukanda wa Gaza.
Mkuu wa ujasusi wa Israel David Barnea kukutana na wajumbe wa Misri na Qatar katika juhudi za kusitisha mapigano Ukanda wa Gaza.Picha: Amir Cohen/REUTERS

Aidha watajadiliana juu ya kubadilishana mateka wa Israel wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza na Wapalestina walio kwenye jela za Israel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mkuu wa shirika la ujasusi la Israel, (Mossad) David Barnea, waziri mkuu wa Qatar Abdulrahman Al-Thani na wajumbe wa Misri wanatarajiwa kukutana leo.

Mazungumzo hayo mjini Doha ni ya kwanza baada ya wasuluhishi kutoka Marekani, Qatar na Misri, kushindwa kuleta suluhisho la kufikia hatua ya kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ulioanza wiki iliyopita.

Wakati huo huo jeshi la Israel limewataka Wapalestina waliopo  kwenye hospitali ya al-Shifa kuhamia upande wa kusini.

Jeshi hilo limewataka Wapalestina waliopo kwenye hifadhi ya hospitali hiyo na vitongoji vyake waondoke kwenye eneo la mapigano wakati wanajeshi wa Israel wanapoingia.

Kwa habari zetu zaidi, tizama vidio yetu ya Habari za Ulimwengu