Mke, mtoto wa rais wa zamani wa Gabon wafungwa miaka 20 jela
12 Novemba 2025
Matangazo
Sylvia Bongo, na mtoto wake, Noureddin Bongo Valentin, walitiwa hatiani bila ya wenyewe kuwapo mahakamani siku ya Jumanne (Novemba 11).
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 62 na mwanawe mwenye umri wa miaka 33 wanaishi uhamishoni nchini Uingereza.
Wawili hao wametiwa hatiani kwa kutumia nafasi zao kumpotosha Ali Bongo kufanya ubadhirifu wa fedha za walipa kodi wa taifa hilo dogo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, lakini lenye umasikini mkubwa miongoni mwa raia wa kawaida.
Bongo, aliyepata maradhi ya kiharusi na kupooza viungo mwaka 2018, alipinduliwa na Jenerali Brice Oligui Nguema tarehe 30 Agosti 2023.
Familia yake nzima iliwekwa kizuizini kwa kipindi cha miezi 20 baada ya hapo.