1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 73 yafukuliwa katika kaburi la pamoja huko Khan Younis

22 Aprili 2024

Miili 73 ya watu imefukuliwa kwenye makaburi ya pamoja karibu na Hospitali ya Nasser huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4f3uO
Mazishi ya watu waliouawa Khan Younis
Wapalestina wakizika miili ya wapendwa wao waliouawa katika vita vya Israel dhidi ya HamasPicha: Mohammed Dahman/AP Photo/picture alliance

Miili 73 ya watu imefukuliwa kwenye makaburi ya pamoja karibu na Hospitali ya Nasser huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kufanya idadi ya miili iliyofukuliwa kufikiwa 283, shirika la Ulinzi wa Raia katika eneo hilo linalodhibitiwa na Hamas limesema. Haijajulikana bado ikiwa miili hiyo ni ya wapiganaji wa Hamas ama raia.

Soma: Takribani watu 17 wauawa katika shambulizi la anga la Israel huko Khan Younis

Jeshi la Israel, IDF limesema linachunguza taarifa hizo, ambazo hazikuweza kuthibitishwa na chanzo huru.

Wanajeshi wa IDF waliingia kwenye hospitali hiyo mnamo mwezi Februari na kuripotiwa kuwauwa watu kwenye hospitali hiyo ambako walihisi kuna magaidi walikuwa wamejificha na kuondoka mapema mwezi huu.