1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

watu 17 wauawa katika shambulizi la Israel huko Khan Younis

Sudi Mnette
5 Machi 2024

Shambulizi la anga la Israel limewaua watu 17 Khan Younis huko Ukada wa Gaza. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa maafisa wa Palestina. Maafisa hao wameongeza kuwa takribani watu 97 wameuawa ndani ya saa 24 zilizopita.

https://p.dw.com/p/4dBnE
Ukanda wa Gaza | Utando wa moshi juu ya Khan Younis
Wapalestina wakitazama helikopta ya Israeli ikiruka juu ya Khan Younis, Ukanda wa Gaza, Alhamisi, Februari 15, 2024.Picha: Mohammed Dahman/AP Photo/picture alliance

Jeshi la Israel limesema katika taarifa yake siku ya Jumanne kuwa limefanya uvamizi na kulenga miundombinu ya wanamgambo mjini Khan Younis wakati likijaribu kuwaondoa raia katika eneo hilo. Wakati huo huo, shirika linaloshughulikia watoto la UNICEF, limesema angalau watoto 10 wanaripotiwa kufa kaskazini mwa Gaza kwasababu ya upungufu wa maji mwilini na utapiamlo. Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Adele Khodr, amesema kuna uwezekano watoto zaidi wanapigania maisha yao katika mojawapo ya hospitali chache zilizosalia Gaza.