Mifumo ya satelaiti ya shirika la utangazaji Iran yadukuliwa
19 Januari 2026
Matangazo
Kanda hiyo ilipeperushwa usiku wa jana katika vituo vingi vinavyorusha matangazo yao kwa kutumia satelaiti ya shirika la utangazaji la Jamhuri hiyo ya Kiislamu ya Iran, lililodhibiti utangazaji wa televisheni na redio.
Video hiyo ilimuonyesha Pahlavi, kisha ikajumuisha kanda ya vikosi vya usalama na wengine walioonekana kuvaa sare za polisi wa Iran.
Ilidai bila kutoa ushahidi kuwa maafisa wengine wa usalama "wameweka silaha zao chini na kula kiapo cha utii kwa watu."Udukuzi huo unakuja huku idadi ya vifo vilivyotokana na maandamano nchini humo ikifikia takriban watu 3,919. Haya ni kwa mujibu wa wanaharakati nchini Iran.