1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Khamenei amshutumu Trump kwa kuchochea maandamano Iran

18 Januari 2026

Kiongozi wa juu zaidi nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei, amemnyooshea kidole cha lawama Rais wa Marekani Donald Trump kwa maandamano ya wiki kadhaa yaliyoambatana na vurugu nchini humo.

https://p.dw.com/p/570VS

Kulingana na shirika la habari la Iran, Khamenei ametoa matamshi hayo Jumamosi na kuongeza kuwa nchi yake inamwona Trump kuwa mhalifu anayehusika na uharibifu, watu kujeruhiwa na kulichafua taifa lake.

Makundi ya haki za binadamu yanasema maandamano hayo yaliyoibuka Desemba 28 kutokana na hali mbaya ya kiuchumi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.

Trump na vitisho kwa serikali ya Tehran

Mara kadhaa, Trump ametishia kuingilia kati kinachoendelea Iran ikiwemo kwa kuchukua hatua kali ikiwa Iran itawanyonga waandamanaji.

Hata hivyo Ijumaa, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Truth Social, Trump aliwashukuru viongozi wa Tehran kwa kuahirisha kuwanyonga waandamanaji. Khamenei kwa upande wake amesisitiza kuwa serikali haitaitumbukiza nchi vitani lakini haitowasamehe wahalifu.

 

Tanbihi ya Mhariri: Makala hii awali ilijumuisha picha kutoka shirika la SalamPix. Iliondolewa tarehe 12 Machi 2026 baada ya Picture Alliance na Imago kutuarifu kuwa walikuwa wanaondoa picha za SalamPix kutokana na wasiwasi kuhusu chanzo chake na uwezekano wa kuwa zimehaririwa.