Merz aonya kuwa Putin anapima subra ya Ulaya
17 Septemba 2025
Matangazo
Akiwahutubia wabunge leo katika bunge la Ujerumani kama sehemu ya wiki ya bajeti, Merz amesema kwa muda mrefu, Putin amekuwa akipima subira ya Ulaya kwa kuhujumu, kupeleleza, kuuwa na kujaribu kuwatatiza watu.
Kansela huyo ameongeza kusema hii imekuwa dhahiri wiki iliyopita nchini Poland, wakati droni za Urusi zilipoingia kinyume cha sheria kwenye anga ya nchi hiyo na kudunguliwa katika eneo hilo kwa mara ya kwanza.
Merz ameonya kuwa Putin alikuwa akitafuta kuyumbisha jamii ya Wajerumani.
Hata hivyo amesisitiza kuwa hawataruhusu hilo kutokea na kusema Ujerumani inaimarisha uwezo wake wa ulinzi .