Merkel amaliza ziara yake Kenya
12 Julai 2011Matangazo
Nchini Kenya, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, anaihitimisha ziara yake rasmi ya siku moja. Bibi Merkel aliwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi na pia kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP, Achim Steiner. Azma na dhamira ya ziara hii rasmi ni kuuimarisha uhusiano na Kenya baada ya Ujerumani kuzindua sera mpya ya mkakati mpya ushirikiano na bara la Afrika hivi karibuni .