Merkel aahidi msaada kwa Ugiriki kabla kura muhimu bungeni | NRS-Import | DW | 28.09.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Merkel aahidi msaada kwa Ugiriki kabla kura muhimu bungeni

Masoko ya hisa barani Ulaya yameimarika kufuatia matumaini mapya yaliyojitokeza kuhusiana na tatizo la madeni linaloikabili Ugiriki, huku thamani ya hisa za Ujerumani na Ufaransa ikipanda kwa asilimia tano.

default

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, kushoto, na waziri mkuu wa Ugiriki, George Papandreou

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ameahidi kuisaidia Ugiriki kwa kila hali kukabiliana na tatizo kubwa la madeni linaloikabili. Bi Merkel alikutana jana na waziri mkuu wa Ugiriki, George Papandreou mjini Berlin, kuzungumzia mzozo huo unaoyumbisha Ugiriki kiuchumi.

Mkutano kati ya viongozi hao umeongeza matumaini ya kuidhinishwa mfuko maalumu kwa ajili ya kuziokoa nchi zinazokabiliwa na madeni katika eneo linalotumia sarafu ya euro. Papandreaou alizuru Berlin siku mbili kabla bunge la Ujerumani, Bundestag, kuupigia kura mfuko huo wa thamani ya euro bilioni 440. Akiwahutubia viongozi wa kibiashara kwenye mkutano wa shirikisho la viwanda la Ujerumani, Papandreou amehakikisha kwamba Ugiriki itaweza kulipa madeni yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com