1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Urusi yawaua watu 11 mjini Kharkiv

Sylvia Mwehozi
20 Mei 2024

Mashambulizi ya Urusi katika mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine yamewaua watu 11 jana Jumapili, kwa mujibu wa mamlaka za eneo la mpakani ambalo linakabiliwa na mashambulizi mapya ya vikosi vya Moscow.

https://p.dw.com/p/4g3ha
Themenpaket Kharkiv Ukraine
Picha: Anadolu/picture alliance

Mashambulizi ya Urusi katika mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine yamewaua watu 11 jana Jumapili, kwa mujibu wa mamlaka za eneo la mpakani ambalo linakabiliwa na mashambulizi mapya ya vikosi vya Moscow. Watu 6 akiwemo mwanamke mjamzito wameauawa nje kidogo ya mji wa Kharkiv katika shambulio la kombora ambalo lilifyatiliwa kutokea mkoa wa Urusi wa Belgorod. Watu wengine 27 wamejeruhiwa na mmoja hajulikani alipo. Muda mchache baadae mamlaka zimeripoti shambulizi jingine ambalo limewaua watu watano.

Tangu Mei 10 vikosi vya Moscow vimefanya mashambulizi ya ardhinikatika mkoa huo wa Kaskazini Mashariki mwa Ukraine, ambako vimeyadhibiti maeneo makubwa katika kipindi cha miezi 18. Ukraine inadai kwamba imevirudisha nyuma vikosi vya Urusi, madai yanayopingwa na Moscow ambayo inasema kuwa inazidi kusonga mbele zaidi upande wa adui.