1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Urusi yaua takriban watu watatu Ukraine

Sudi Mnette
18 Februari 2024

Takriban watu watatu wameuawa kwa droni na mashambulizi ya makombora ya Urusi mashariki mwa Ukraine,.

https://p.dw.com/p/4cXfc
Ukraine | Shambulio la roketi la Urusi huko Kramatorsk
Kikosi cha zimamoto kikijaribu kuzima moto kwenye jengo lililoharibiwa na shambulio la roketi la Urusi huko Kramatorsk, Ukraine mnamo Agosti 15, 2023. Picha: Jose Colon/AA/picture alliance

Kwa mujibu wa taarifa ya leo ya viongozi wa maeneo hayo miili miwili hadi sasa imepatikana kutoka kenye kifusi cha jengo la makazi katika mji wa Kramatorsk ambalo lilipigwa na kombora la usiku. Kupitia ukurasa wake wa telegram kiongozi wa kijeshi katika eneo hilo, Vadym Filashkin amesema shughuli ya uokoaji inaendelea na waathiriwa zaidi wanashukiwa kuwa chini ya vifusi. Nae Oleh Syniehubov, mkuu wa utawala wa kijeshi katika eneo jirani, Kharkiv amesema mtu mmoja amekufa na watano kujeruhiwa katika shambulio la jengo la makazi la ghorofa huko Kupiansk. Katika mji mwingine jirani wa Sloviansk, shuleimeshambuliwa vibaya. Waokozi wapo katika juhudi za kuwatafuta waaathirwa na hasa watu wanaweza kuwa wamenasa katika mabaki ya majengo.