1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Marekani yatathmini mustakabali wa operesheni zake Sahel.

18 Machi 2024

Hatua hiyo inafuatia tangazo la serikali ya Niger kuwa inasitisha ushirikiano wake wa kijeshi wa miaka mingi na Washington.

https://p.dw.com/p/4dqDu
Makomando wa jeshi la anga la Marekani wakifanya mazoezi kuhusu matumizi ya droni Niger
Makomando wa jeshi la anga la Marekani wakifanya mazoezi kuhusu matumizi ya droni NigerPicha: Alex Fox Echols Iii/Planetpix/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Serikali ya Niger ilitoa tangazo hilo baada ya ziara ya maafisa wakuu wa Marekani nchini humo.

Eneo hilo limekuwa likisumbuliwa na makundi ya wapiganaji walio na itikadi kali wanaohusishwa kuwa na mahusiano na makundi ya al-Qaida na lile linalojiita Dola la Kiislamu IS.

Mjumbe mkuu wa Marekani Molly Phee alirejea katika mji mkuu wa Niger, Niamey, wiki hii kukutana na viongozi waandamizi wa serikali, akiambatana na mkuu wa Kamandi ya ya jeshi la Marekani Afrika Jenerali Michael Langley.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema siku ya Jumapili kupitia mtandao wa X kwamba mazungumzo yalikuwa ya uwazi na kwamba inawasiliana na viongozi wa kijeshi.

Haikuwa wazi ikiwa Marekani bado inayo nafasi yoyote ya kufikia makubaliano ya kusalia nchini humo.