1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani imeharibu kombora la ardhini-angani la Wahouthi

2 Machi 2024

Vikosi vya Marekani vimeshambulia na kuharibu kombora la kufyatuliwa ardhini kwenda angani la waasi wa Kihouthi wa nchini Yemeni, baada ya kuamua kuwa linato kitisho kwa ndege za Marekani.

https://p.dw.com/p/4d6Mo
Jeshi la wanamaji Marekani likifyatua kombora kulenga vituo vya Wahouth
Jeshi la wanamaji Marekani likifyatua kombora kulenga vituo vya Wahouth Picha: U.S. Central Command/Handout via REUTERS

Kamandi ya Jeshi la Marekani katika Kanda ya Mashariki ya Kati imesema kuwa siku ya Ijumaa Wahouthi walirusha kombora la kushambulia meli kwenye Bahari ya Shamu lakini hakukuwa na uharibifu wowote.

Juma lililopita vikosi vya Marekani na Uingereza vilifanya mashambulizi dhidi ya vituo 18 vya Wahouthi katika maeneo manane nchini Yemeni, ikiwa ni pamoja na vituo vya kuhifadhia silaha. Kwa mujibu wa Wahouthi mashambulizi hayo yalisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wanane walijeruhiwa.

Soma pia:Marekani: Vikosi vya Iran na Hezbollah vinawasaidia Wahouthi

Waasi wa Houthi ambao wanaungwa mkono na Iran wamekuwa wakishambulia meli katika Bahari ya Shamu tangu Novemba katika kampeni wanayosema ni kuonesha mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.