Marekani bingwa wa mpira wa kikapu ulimwenguni | Michezo | DW | 15.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Marekani bingwa wa mpira wa kikapu ulimwenguni

Marekani imeibwaga Serbia katika fainali na kushinda Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu. Marekani imeirambisha Serbia vikapu 129 kwa 92 na kuwa timu ya kwanza kulitetea taji lao tangu mwaka wa 2002

Angola na Senegal ziliiwakilisha afrika lakini mambo yalizidi unga na zikaondolewa mapema katika dimba hilo. Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la Mwaka huu wa 2014 lilikuwa toleo la 17 la Shirikisho la Mpira wa Kikapu Ulimwenguni - FIBA Basketball World Cup.

Hapo awali michuano hiyo ilifahamika kama FIBA World Championship. Michuano hii iliyofanyika Uhispania ndiyo ya mwisho kuandaliwa katika mzunguko wa miaka minne kwa sababu michuano ijayo itafanyika miaka mitano ijayo nikiwa na maana kuwa mwaka 2019 ili kurekebisha hesabu za miaka kuingilia ratiba ya Kombe la Dunia na FIFA.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu