Mapigano yazuka tena kivu kaskazini mashariki mwa Kongo | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mapigano yazuka tena kivu kaskazini mashariki mwa Kongo

Maelfu ya raia wametoroka makaazi yao kufuatia kutibuka kwa mapigano makali hii leo mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kati ya wanamgambo na waasi wanaongozwa na Generali muasi Laurent Nkunda

Generali muasi Laurent Nkunda

Generali muasi Laurent Nkunda

Umoja wa mataifa na jeshi la Kongo wamesema mashambulio mabaya yametokea mapema leo katika eneo la Bunagana mji ulioko kiasi kilomita 50 kaskazini mashariki mwa Goma mji mkuu wa mkoa wa Kivu kaskazini.Kamanda wa jeshi la Kongo Delphin Kahimbi amesema habari walizozipokea zinasema mapigano hayo yanawahusisha wanamgambo wa Mai Mai kutoka Kasereka na wafuasi wa Nkunda.

Msemaji wa kikosi cha Umoja wa mataifa Monuc Sylvie Van Den Wildenberg amesema maelfu ya raia waliojawa na hofu wamekimbilia eneo la Rutshuru kaskazini magharibi mwa Kongo.

Wakati huohuo Uganda imesema imeimarisha vikosi vyake katika mpaka wake na Kongo katika eneo hilo la mapigano ili kujiweka tayari kukabiliana na vikosi vya Nkunda endapo vitaingia eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com