Maoni: EU yajaribu kuweka hai mkabata wa kinyuklia na Iran
18 Mei 2018Mataifa ya Umoja wa Ulaya yamechukua hatua kuyaruhusu makampuni ya Ulaya kukwepa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran katika kile kinachojulikana kama "sheria inayozuwia".
Tofauti na wakati huu, wakati ule rais wa Marekani alikuwa Bill Clinton, lakini leo inajulikana. Pamoja na hayo Umoja wa Ulaya unaweza kuyalinda makampuni yake dhidi ya kitisho cha vikwazo vya Marekani na kuzuwia athari zake.
Pia uwekezaji rasmi ama misaada rasmi kupitia uwekezaji wa makampuni ya binafsi unawezekana. Umoja wa Ulaya pia kupitia vyombo hivyo unaweza kuingia katika mapambano na Trump.
Ni kwa njia hiyo tu makampuni ya Ulaya yanaweza kufanyakazi, katika nchi ambayo inalengwa na Marekani katika mtazamo wake kama inavyoonekana kwa Iran. Sasa linabakia swali tu iwapo mataifa ya Ulaya na viongozi wao wako tayari kuingia ulingoni kuitetea Iran.
Kila konde la nguvu litakalotoka upande wa Umoja wa Ulaya kuelekea Marekani linaweza kuzidisha mapambano zaidi, na kuelekeza katika uharibifu mkubwa zaidi wa kiuchumi. Hata ilipofika Jumanne jioni hakukuwa na ishara ya matumaini makubwa, kwamba viongozi wa Ulaya wako tayari, kuelekea katika njia hii.
Makampuni yanauchaguzi
Kwa hali hiyo makampuni makubwa ya kibiashara kama Siemens yanatarajia kuchukua uamuzi, kama kufanyakazi na Iran ama kuwekeza zaidi na kujiingiza katika mgogoro na Marekani. Huenda pengine ikawa fursa sahihi kwa ajili ya mwelekeo wa makampuni hayo, kwamba biashara na Marekani kwa wengi ni muhimu sana.
Kwa upande wa kampuni la Siemens kwa mfano Marekani ndio soko lake kuu. Kwa Umoja wa Ulaya huu ni utata mkubwa, kwani wanahitaji makampuni ya watu binafsi, kuweza kufanikisha uwekezaji nchini Iran, uwekezaji ambao unahitajika mno. Lakini Umoja wa ulaya hauwezi kuyalazimisha makampuni, kufanyakazi nchini Iran. Mataifa yaliyobaki ambayo yalitia saini makubaliano ya kinyuklia na Iran, bado yanajaribu kutafuta njia.
Lakini hata hivyo kuna matatizo. Urusi kwa mfano inataka kutekelezwa kwa kina makubaliano hayo, wakati kiuchumi ni mshindani mkubwa wa Iran. Mataifa hayo yote yanategemea sana biashara ya nje ya mafuta. Na kwa upande wa China kwa kweli ina mambo yake ya kufanya badala ya kujiingiza katika mapambano katika jambo hili na Marekani.
Kwa hivi sasa China inajaribu kuzuwia vita vya kibiashara na utawala wa Trump. Katika suala hili la mkataba na Iran kwao lina umuhimu mdogo.
Mwandishi: Max Hofmann / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Josephat Charo