1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia wapinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Niger

22 Aprili 2024

Mamia ya watu wameandamana ili kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Niger, huku ujumbe kutoka Washington ukitarajiwa kuwasili nchini humo siku chache zijazo.

https://p.dw.com/p/4f2az
Niger Maandamano-Niiamey
Maandamamno ya mjini Niamey kupinga uwepo wa wanajeshi wa MarekaniPicha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Mamia ya watu wameandamana hapo jana ili kupinga uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Niger, huku ujumbe kutoka Washingtonukitarajiwa kuwasili nchini humo siku chache zijazo ili kupanga mikakati ya kujiondoa katika taifa hilo linalotawaliwa na jeshi.

Maandamano hayo yalishuhudiwa katika mji wa kaskazini mwa jangwa wa Agadez, kunakopatikana kituo cha anga cha Marekani, na yaliitishwa na kundi la vyama 24 vya kiraia ambavyo vimMarekani yasitisha msaada kwa Niger huku vikosi vya Ufaransa vikianza kuondokaekuwa vikiinga mkono serikali ya kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka jana.

Soma pia: Marekani yasitisha msaada kwa Niger huku vikosi vya Ufaransa vikianza kuondoka

Marekani iliafiki siku ya Ijumaa kuwaondoa wanajeshi wake zaidi ya 1,000 katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ambako Marekani ilijenga kambi yake kubwa ya kijeshi yenye thamni ya dola milioni 100 ambayo pia ilikuwa ikitumiwa kurusha droni zake.