Makali ya sheria ya usalama yaanza kushuhudiwa Hong Kong | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Makali ya sheria ya usalama yaanza kushuhudiwa Hong Kong

Polisi ya Hong Kong leo hii imewasilisha mashitaka yake ya mwanzo kabisa kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya usalama ya China, ambayo imeanza kutumika rasmi mapema wiki hii katika jiji hilo.

Taarifa ya polisi inasema kijana wa umri wa miaka 24, anashitakiwa kwa makosa mawili, ambapo la kwanza linahusu uchochezi na lingine la uanaharakati wa kigaidi. Aidha taarifa hiyo ilifafanua zaidi kwa kusema mashataka hayo yanamuhusu kijana huyo ambae aliendesha pikipiki kwa kuelekea upande wa maafisa wa polisi katika harakati za maandamano ya kuipinga sheria ya usalama, katika tukio ambalo polisi imesema maafisa wake watatu walijeruhiwa.

Katika hatua nyingine mwanaharakati maarufu wa Hong Kong, Nathan Law ameondoka katika jiji hilo, na kwenda kusikojulikana, baada ya kuanza makali ya utekelezaji wa sheria ya usalama. Hayo ameyabainisha katika ukurasa wake wa Facebook, ikiwa baada ya kutoa ahadi ya kutoa ushahidi wake wa hali ya mambo mjini Hong Kong kwa bunge la Marekani.

Sheria mpya yawatia nguvuni watu 370

Hongkong Nathan Law, Aktivist

Mwanaharakati wa Hong Kong Nathan Law

Jumatano iliyopita polisi ya jiji hilo iliwatia nguvuni watu 370, ikiwa 10 miongoni mwa hao, wamewekwa kizuizini kwa njama za kuihujumu sheria ya usalama, pale ambapo maelfu ya watu waliingia mitaani kupinga.

Aidha Kansela wa Ujerumani, Angeka Merkel amesema Umoja wa Ulaya lazima uzungumze kwa kauli moja kuhusu China, akioneshaa wasiwasi wake kuhusu sheria mpya ya usalama. Naye Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesema Uingereza lazima ishikamane na watu wa Hong Kong. Nathan Law ni mpigania demokrasia.

Soma zaidi:Umati waandamana Hong Kong kupinga mpango wa kuwashtaki watuhumiwa China

Serikali ya China imemteuwa mratibu wake mkuu wa kisera wa Hong Kong, Carrie Lam kuwa mshauri wa sheria ya ulinzi katika kufanikisha utekelezaji wa sheria mpya ya usalama wa taifa hilo. Kamati hiyo itakuwa na majukumu ya kutoa muongozo na kutekeleza sera, kwa zingatio za sheria hiyo ambayo imeanza kutelezwa mapema wiki hii. Na afisa mwingine wa ofisi ya juu kabisa chama cha kimunisti Luo Hiuning ameteuliwa kuwa kuwa mshauri mkuu wa masuala ya usalama.

Wakati huo huo, Zheng Yanxioon, afisa wa China kutoka jimbo la Guangdong, ataongoza ofisi mpya chama cha Kikomunisti ya Hong hong, kwa ajili kufuatilia hali ya mambo inavyoendeshwa katika eneo hilo. Zheng anajulikana sana kwa namna yake alivyowashughulikia kimababvu waandamanaji katika Wukan, huko katika jimbo la Guangdong mashariki mwaka 2011.