1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Katiba Afrika Kusini yampiga Stop Zuma

20 Mei 2024

Uamuzi huo umezua hofu ya kutokea machafuko makali kuelekea uchaguzi, ambao tayari ni wenye ushindani mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa demokrasia mwaka 1994.

https://p.dw.com/p/4g4rZ
Afrika Kusini| Mahakama yamzuwia Zuma kuwania katika uchaguzi mkuu
Wafuasi wa chama cha Zuma wakiwa nje ya mahakama baada ya umuazi wa kumzuwia kuwania ubunge.Picha: MARCO LONGARI/AFP

Mahakama ya juu nchini Afrika Kusini imetoa uamuzi wake leo Jumatatu wa kumpiga marufuku rais wa zamani Jacob Zuma kugombea katika uchaguzi wa bunge utakaofnyika wiki ijayo kwa sababu kwamba alipatikana na hatia ya kuidharau Mahakama mwaka 2021 na hilo ndilo lililodhibiti ushiriki wake katika uchaguzi huo.

Soma pia: Zuma hastahili kugombea katika uchaguzi mkuu Afrika Kusini

Korti ya katiba iliamua kuwa kufuatia  Zuma kupewa kifungo cha miezi zaidi ya12  jela kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake ya tuhuma za kuhusika na rushwa imemfanya kutokuwa na uhalali wa kushiriki uchaguzi huo.

Mwezi wa Januari chama chake cha zamani ambacho ndio chama tawala cha African National Congress ANC killisimamisha uanachama wa Zuma aliye na miaka 82. Na tangu wakati huo aliunda chama chake cha Umkhonto we Sizwe (MK) na alitarajia kusimama kama mwenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi wa May 29.