1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya juu yaidhinisha marufuku ya kusafiri ya Trump

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2018

Mahakama ya juu nchini Marekani imeidhinisha marufuku ya kusafiri, iliyotolewa na rais Donald Trump ikiyalenga mataifa yaliyo na idadi kubwa ya Waislamu.

https://p.dw.com/p/30MIz
USA Trumps Einreiseverbot
Picha: Getty Images/AFP/F. J. Brown

Mahakama ya juu nchini Marekani imeidhinisha marufuku ya kusafiri, iliyotolewa na rais Donald Trump ikiyalenga mataifa yaliyo na idadi kubwa ya Waislamu. Mahakama hiyo ilitoa uamuzi wake siku ya Jumanne na kusema kwamba marufuku ya Trump, haivunji sheria za uhamiaji za Marekani.

Jaji mkuu John Roberts, aliandika katika maoni yake kwa mahakama kwamba rais, aliweka utetezi wa kutosha kuhusu usalama wa taifa kwa kuwazuia watu wengi wanaoingia Marekani, kutoka Somalia, Iran, Yemen, Syria, Libya, Chad, Korea Kaskazini na Venezuela.

Hata hivyo aliongeza kwamba mahakama haina mtizamo wowote juu ya uwazi wa sera. Uamuzi huo unadhihirisha kile kinachoonekana kuwa ushindi mkubwa wa kwanza wa sera za Trump tangu aingie madarakani Januari 2017.

Katika taarifa yake, Trump amesema uamuzi huo ni uthibitisho na ushindi mkubwa kwa watu wa Marekani.