1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin: Matamshi ya Biden yameidhalilisha Marekani

Lilian Mtono
22 Februari 2024

Ikulu ya Kremlin mapema leo imeyakosoa matamshi yaliyotolewa na Rais Joe Biden wa Marekani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo, Vladimir Putin na kusema yameidhalilisha serikali ya Marekani na wale wanaotumia msamiati huo.

https://p.dw.com/p/4cjcQ
Marekani | Rais Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Biden kwenye hafla ya kukusanya fedha huko mjini San Francisco hapo jana alimfananisha Putin na mwendawazimu, huku akionya juu ya kitisho kilichopo wakati wote cha nyuklia, ingawa kwa upande mwingine akisema kitisho kikubwa dhidi ya ubinaadamu kinabakia kuwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Soma pia:Biden, Scholz kujadiliana msaada kwa Ukraine

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema matumizi ya lugha kama hiyo ya rais wa Marekani dhidi ya kiongozi wa taifa jingine hayampunguzii mamlaka rais Putin bali kuwafedhehesha wale wanaoitumia na Marekani kwa ujumla wake.