Kesi yaendelea dhidi ya waasi wa ADF | Matukio ya Afrika | DW | 16.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kesi yaendelea dhidi ya waasi wa ADF

Kesi dhidi ya waasi wa Uganda wa kundi la ADF wanaoshukiwa kuwaua watu kwa kuwakata kwa mapanga katika mji na wilaya ya Beni inaendelea.

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya mahakama katika eneo hilo, Meya Bwanakawa Masumbuko Nyonyi alieko madarakani na ambae hajasimamishwa kazi atafikishwa kizimbani kutoa ushahidi baada ya kushukiwa kuwa ni mmoja wa viongozi wa kundi la kigaidi ADF. Kamanda wa ADF aliyemtaja Meya huyo kuwa ni mmoja wa viongozi wa ADF, alimtaja pia Jenerali Mundos, aliekuwa pia kamanda wa operesheni za kijeshi dhidi ya kundi  hilo  la  ADF katika mji na wilaya ya Beni, pale yalipoanza mauwaji ya raia kwa kukatwa kwa mapanga. Raia zaidi ya elfu moja na mia tano  wameuawa na  wanamgambo  wa  kundi  la  ADF, kwa mjibu wa takwimu za mashirika ya kiraia.