1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroVatican

Kanisa Katoliki duniani lalaani mauaji katika ukanda wa Gaza

7 Oktoba 2025

Mwanadiplomasia mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Pietro Parolin amelaani "mauaji yanayoendelea" katika ukanda wa Gaza - hii ikiwa moja ya shutuma kali zaidi kutoka Vatican dhidi ya Israel katika vita vyake na Hamas.

https://p.dw.com/p/51cGW
Vatikan | Papa | Kadinali Pietro Parolini
Katibu wa serikali ya Vatican na msaidizi wa karibu wa kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV, Pietro ParolinPicha: TIZIANA FABI/AFP/Getty Images

Katika mahojiano yaliyofanyika kuhusiana na kumbukumbu ya miaka miwili tangu shambulio la Hamas, kadinali Parolin pia amelaani mashambulizi ya kundi la Hamas na kuyataja kuwa "ya kinyama na yasiyoweza kutetewa" huku akitoa wito kwa Hamas kuwaachilia huru mateka waliobaki.

Parolin ambaye ni katibu wa serikali ya Vatican na msaidizi wa karibu wa kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV, amesisitiza kuwa watu wanaoshambuliwa wana haki ya kujilinda, lakini lazima hatua za kujilinda ziheshimu kanuni ya uwiano.

Ubalozi wa Israel katika Makao Makuu ya Kanisa Katoliki umetoa tamko ukieleza kwamba mahojiano ya Parolin "bila shaka yalikuwa na nia njema," lakini mahojiano hayo yamekosolewa kwa madai kuwa yalilenga zaidi kuikosoa Israel huku yakipuuza hatua ya Hamas kukataa kuwaachilia mateka au kusitisha ghasia.